10 Julai 2016 - 18:06
Daesh wachoma moto visima vitano vya mafuta nchini Iraq

Kikundi cha kigaidi cha Daesh chachoma moto visima vitano vya mafuta nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Daesh kimechoma moto visima vitano vya mavuta katika sehemu ya Algayyarah kusini mwa wilaya ya Mosul nchini Iraq
Kikundi hicho cha kigaidi kimechukua hatua hiyo baada ya kukombolewa kambi ya jeshi la anga na uwanja wa ndege wa kijeshi wa Qayyarah na kusambaratishwa magaidi hao katika sehemu hiyo na baada kushindwa kuithibiti sehemu wakaamua kuchoma moto visima vitano vya mafuta na baadaye kumbia na familia zao, uchomaji wa visima hivyo umedhihiri baada ya moshi mzito kuonekana kusambaa katika sehemu hiyo.
Waziri mkuu wa Iraq “Haidar Al-Abadiy” siku ya Jumamosi ametangaza rasmi kukombolewa  kwa kambi hiyo ya Qayyarah nakusema kuwa kambi hiyo ya jeshi la anga la Iraq ndio sehemu itakayo tumika kuanza mashambulizi ya kuikomboa wilaya ya Mosul nchini humo.
Kambi ya jeshi la anga ya Qayyarah iko nje kidogo ya wilaya ya Mosul, ambayo ndio kambi kubwa ya jeshi la Iraq iliopo kaskazini mwa nchi hiyo.
Wilaya ya Mosul toka miaka miwili iliopita mpaka sasa iko chini ya kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo katika wilaya hiyo hutumika kanuni za kikundi hicho cha kigaidi wilayani humo.
mwisho wa Habari/290